IVANA ashtua mashabiki wa soka..... Niko single

 


Shabiki wa soka anayetajwa kuwa na mvuto zaidi, mrembo Ivana Knoll ameshtua watu baada ya kuwaambia kwamba atakwenda kushangilia fainali za Euro 2024 zitakazofanyika huko Ujerumani akiwa singo, hana mtu yeyote.

Mrembo Ivana Knoll amekuwa maarufu kwenye majukwaa ya mashabiki kutokana na vivazi vyake na mwili wake wenye mvuto mkubwa, huku mara zote amekuwa akionekana akiwa kwenye mavazi ya bendera ya timu yake ya taifa ya Croatia.

Miss Croatia wa zamani alisema atakwenda Ujerumani kuishangilia timu yake ya taifa ya Croatia baadaye mwezi huu akiwa hana mwanamume yeyote. Hata hivyo, mrembo Ivana alionekana kuweka ngumu kwa wanaume yeyote atakayekwenda Ujerumani kwa lengo la kwenda kujaribu bahati yake kwa mrembo huyo.

Mrembo Ivana alisema: “Nilikuwa na mpenzi yake ambaye tulikuwa pamoja kwa miaka 10. Tuliachana mwaka jana. Kwa sasa nipo singo, lakini wala sihitaji mwanaume kwa kipindi hiki.