H.BABA Arudi kwa Harmonize

 


Mwaka jana/juzi H.BABA alijitoa kwenye uanafamilia wa Konde gabf na kuhamia Wasafi ya Diamond.

Wakati anaondoka kwa Harmonize alitoa maneno mengi machafu na udhalilishaji huku akimsifia Diamond Plutnum kwa kumuomba msamaha na kumsujudia miguuni..

Baada ya mambokwenda ndivyo sivyo tofauti na matarajio yake, familia ya Diamond plutnum imekuwa ikionyesha kutokuwa na muda naye na kumnyima upenyo wa kula chungu kimoja. H.BABA ameamua kurejea kwenye kambi yake ya awali ya Konde gang. Bila hiyana Harmonize amekubali kumpokea kwa mikono miwili baada ya kumpigia magoti na kujutia maamuzi yake ya kuisaliti kambi ya Konde gang.